Nimewatumia Rafiki Elimu ujumbe wa kuwajibu kuwa ninawashukuru kwa kitumia wavuti.com kufikisha taarifa na matangazo mbalimbali kwa jamii, kwa mfano hii ya kumtafuta mtuhumiwa wa utapeli iliyopachikwa hapa.
Ni matumaini ya wavuti.com kuwa Rafiki Elimu Foundation na mtuhumiwa, watatendewa haki kwa mujibu wa sheria.
Habari za leo dada Subira, uongozi wa RafikiElimu Foundation unapenda kutoa shukurani za dhati kwako na kwa blogu yako kwani kuandikwa kwa taarifa kuhusu mtuhumiwa aliyekuwa anafanya utapeli mtandaoni kwa jina la taasisi yetu kumesaidia kutiwa hatiani kwa mtu huyo. Mtu huyo ametiwa hatiani siku ya juzi tarehe 14 MEI 2013 mjini Njombe na anashikiliwa katika kituo cha polisi Njombe akisubiri kuletwa Dar es Salaam kwa ajili ya kufikishwa mahakamani. Tunashukuru sana sana sana na sana.
Kwa niaba ya viongozi wenzangu,
Yusuf Djibril,
Mkurugenzi Msaidizi,
RafikiElimu Foundation.
Bofya hapa kwa maelezo zaidi
ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU...
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Acp Fulgency Ngonyani amethibitishwa kukamatwa kwa tapeli huyo na kwamba kwa sasa alikuwa akifanya kazi kama Project Coordinator wa Agape Foundation, asasi isiyo ya Kiserikali inayoshughulikia masuala ya watoto yatima wilayani Njombe.
Kamanda Ngonyani amesema Mtuhumiwa Huyo kama Jina lake Linavyojieleza kwenye tangazo na picha zake mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa SIDO Njombe amekamatwa juzi tarehe 14.05.2013 majira ya jioni na hatua za kumsafirisha kupelekwa makao makuu ya Polisi Jijini Dar es Salaam zinaendelea kutokana na kesi yake kufunguliwa huko.
Aidha amesema kuwa hadi sasa wanamsubiri Askari atakayetumwa kutoka Makao Makuu Jijini Dar kuja kumchukua.
Taarifa za awali zilieleza kutafutwa kwa tapeli huyo toka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment