Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imeweka
mkakati madhubuti wa kuwapatia wakulima mbegu na mbolea kwa utaratibu
ulio bora na wenye maslahi mapana, Bunge lilielezwa jana.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika, Adam Malima ambaye alisema kuwa mkakati huo
utatokana na ushauri wa kitaalamu wa kutoka kwa watalaamu wa ngazi zote
wakiwamo wakulima, watafiti, wagani na mawakala wa mbolea.
Alikuwa akijibu swali la Athuman Mfutakamba
(Igalula-CCM) aliyehoji juu ya Serikali kuwapatia wakulima wa maeneo ya
Uyui mbegu bora na kuwabadilishia kutoka mbegu za zamani na kuwapatia
mbegu za mahindi aina ya DKC 8053.
Malima alisema kuwa utaratibu uliopo ni kwa
wakulima wa halmashauri husika kuwasilisha wizarani mahitaji halisi ya
aina ya mbegu za mahindi wanazopendelea.
Kuhusu utaratibu wa utoaji wa ruzuku ya pembejeo
kwa utaratibu wa vocha, alisema wakulima hunufaika kwa kupatiwa seti ya
vocha tatu za mbolea ya kupandia.
Mbali na mbegu za mahindi lakini alisema wakulima
kwa baadhi ya maeneo hupewa mbegu bora za mpunga ambapo wakulima wa eneo
husika huchagua mbegu wanayoihitaji baada ya kushauriwa na maofisa
ugani.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment