Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao chake na
wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House,
Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge
Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa
Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip
Mangula.
Wabunge wa CCM wakiwa kwenye kikao chao na Mwenyekiti wa CCM Rais
Jakaya Kikwete leo kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya
CCM mjini Dodoma.
Wajumbe
kwenye kikao cha Mwenyekiti wa CCM na Wabunge wa CCM na Mwenyekiti wa
CCM Rais Jakaya Kikwete wakibadilishana mawazo ukumbini. Walioketi
mbele, Kushoto ni Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakiah Meghji na Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migoiro na Mbunge wa Urambo na
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini wakati wa
kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo
la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni
Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama
na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo
na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC
Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata wakati wa
kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Same Anne Kilango Malecela.
Mbunge wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk. Emmanuel Nchimbi
(kushoto) akitaniana kuhusu Uyanga na Simba na Mwenyekiti wa Simba,
Mbunge wa Tabora Aden Rage nje ya ukumbi kabla ya kuanza mkutano huo.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya.
Chanzo: Bashir Nkoromo
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment