Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo asubuhi ,(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa Kitaalamu wa Chuo cha Ardhi serikali ya Muungano Dk.Staulans Ntiyakunze,(wa tatu kulia) baada ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo asubuhi ,(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia meza na vikalio vyake wakati alipotembelea moja ya madarasa katika Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo, baada ya kuzindua Chuo hicho,(kushoto) Mkuu wa Chuo Dk. John Magoti, na pili kulia makamo wa kwanza wa Rauis wa Maalim Seif Sharif,akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk.Salim Ahmed Salim.
Mwalimu wa Darasa la Kompyuta Julius Maungo,akitoa
maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea katika darasa la kompyuta leo baada ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo asubuhi ,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Dk. John Magoti, baada ya kuzindua rasmi Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,huko Bububu Zanzibar leo asubuhi alipotembelea sehemu
mbali mbali za Chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa Chu cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere Tawi la Zanzibar wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa chuo hicho leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea zawadi kutooka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mwalimu Nyerere Dk.Salim Ahmed Salim,wakati wa uzinduzi wa Tawi la Chuo hicho uliofanyika leo huko Bububu Nje ya Mji wa Zanzibar,
[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohmed Shein
amevitaka vyuo nchini kutolegeza vigenzo vya udahili wa wananfunzi
wanaojiunga na vyuo hivyo kwani kufanya hivyo kunaweza kuathiri ubora wa
elimu na taaluma inayotolewa.
Dk.
Shein amesema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere lilopoto Bububu nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
“Tusilegeze
masharti au vigezo vya wananfunzi kujiunga na vyuo kwa sababu kufanya
hivyo kunaweza kuathiri ubora wa taaluma inayotolewa na kusababisha
heshma ya chuo kushuka” alieleza
Alifafanua
kuwa pamoja na kuwepo na vyuo vingi nchini hivi lakini wanafunzi wengi
wanakimbilia katika vyuo vinavyotambuliwa kwa kutoa elimu bora na
wataalamu wenye uwezo katika taaluma zao na wanaoweza kushindana katika
soko la ajira.
“Uzuri
wa taasisi ya elimu haupimwi kwa kuangalia ubora wa mazingira
yanayotolewa elimu pekee bali hupimwa kwa uwezo wa taaluma wanayokuwa
nayo wahitimu wake hivyo taasisi ya Mwalimu Nyerere lazima izingaite
ubora wa maarifa ya wahitimu wake”alisisitiza.
Kwa
hivyo aliitaka Menejimenti na Bodi ya chuo hicho iliyo chini ya
uenyekiti wa Dk. Salim Ahmed Salim kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa
katika chuo hicho inalingana sio tu na historia ya chuo bali hadhi ya
jina la Mwalimu Nyerere.
Rais
wa Zanzibar ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kugharimia ujenzi wa chuo hicho ambao umegharimu zaidi ya shilingi ya
bilioni 6.
Alisema
fedha hizo zimewezesha kutekeleza Sheria Namba 6 ya mwaka 2005 ya
kuanzisha Taasisi hiyo ambayo iliekeleza Taasisi hiyo iliyo na makao
Mkauu yake Tanzania Bara kuwa na Tawi lake Zanzibar.
“Sheria
hiyo(Namba 6) inatamkia wazi kwamba chuo kitakuwa na Tawi Zanzibar. Kwa
kuwa Sheria ni jambo moja na utekelezaji Sheria inayohusika ni jambo
jingine, napenda kuipongeza Bodi ya Chuo kwa kusimamia vyema utekelezaji
wa Sheria iliyoanzisha chuo” alieleza.
Kwa
upande wake Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar
itajitihadi kila inapowezekana kuziunga mkono jitihada za Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza ujenzi wa Tawi hilo la
chuo.
“Katika
kutoa mchango wake Serikali itaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano
ili kuhakikisha kuwa changamoto zinazokikabili chuo hiki zinapatiwa
ufumbuzi hatua kwa hatua”alibainisha.
Amewataka
vijana kuitumia fursa ya kuwepo kwa chuo hicho kujiendeleza kitaalamu
badala ya kuendekeza mambo yasiyohusiana na masomo yao kama masuala ya
siasa na migogoro ya dini pamoja na kuiga tamaduni za nje.
“Kwa
bahati baadhi ya vijana wanapojiunga na vyuo hasa vya elimu ya juu
hujisahahau na kuiga mambo yasiyolingana na utamaduni wetu,silka zetu na
yaliyo kinyume na maadili yetu” alisema hivyo sivyo na kuongeza kuwa
wanaofanya hivyo wanajiharibia maisha yao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Dk. Salim Ahmed Salim aliieleza
jumuiya ya wananchuo na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa Taasisi
yake imefurahishwa na jinsi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
inavyoithamini Taasisi yake.
Hivyo
ametoa wito kwa vijana kote nchini na husan wa Zanzibar kuitumia fursa
hiyo kupata taaluma mbalimbali zinakazolisaidia taifa kupiga hatua
kimaendeleo.
“Mkiitumia
fursa hii vyema wakati huu wa utandawazi mtakuwa mmejifanyia mema
nyinyi wenyewe na taifa lakini msipoitumia vizuri tutakula hasara
kubwa”alisisitiza.
Nae
Mkuu wa Chuo hicho Dk. John Magoti aliishukuru Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kwa kuipatia hekta 81.8 ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa chuo
hicho.
Akisoma
taarifa ya ujenzi na majukumu ya chuo Dk. Magoti alieleza kuwa mpango
wa Taasisi ni kuongeza majengo mengine mawili ili kukidhi mahitaji
halisi ya nafasi kwa shughuli za utawala pamoja na masomo.
Alitaja
changamoto zinazoikabili taasisi hiyo kuwa ni pamoja na ufinyu wa
bajeti,ukosefu wa hosteli kwa wanafunzi, idadi ndogo ya udahili na
vijana wa Zanzibar kutochangamkia nafasi za ajira wakati Taasisi hiyo
inapotangaza nafasi hizo hivyo kusababisha wakufunzi wengi kuwa wametoka
Tanzania Bara.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment