Ikulu
Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mheshimiwa
Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatano,
Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa
taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa
kukaa madarakani”.
Ukweli ni
kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa
mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015
kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa na kumpa nafasi ya kustaafu
mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa taifa letu.
Katika habari
hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda” Mheshimiwa Lipumba
anadai kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete “ itakaa
madarakani hadi mwaka 2017” kwa
sababu kuna “wasiwasi kuwa mchakato wa
sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014.”
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa taarifa hiyo ya Mheshimiwa Prof.
Lipumba ni uzushi mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi. Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango
hiyo.
Taarifa hiyo
imedokeza kuwa itakuwa ni vyema kwa Mheshimiwa
Lipumba kuisaidia jamii kusema nani
anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane.
Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha
tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria mambo
yasiyokuwepo.
0 comments:
Post a Comment