MHASHAM Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, NORBERT WENDELIN MTEGA.
Taarifa hizo zimetolewa na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania leo mchana
kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambapo amesema kuwa Baba Mtakatifu FRANCIS
amekubali kisheria ombi la kustaafu kwa mhashamu askofu mkuu wa jimbo
kuu katoliki la Songea.
Nafasi yake kwa sasa imekaimishwa kwa askofu TARCISIUS
NGALALEKUMTWA (ASKOFU WA JIMBO LA IRINGA NA RAIS WA TEC) ambaye atakuwa msimamizi wa Jimbo Katoliki la Songea.
Sababu za kustaafu zimetajwa kuwa ni kutokana na tatizo la kiafya ambalo limekuwa likimkabili kwa kipindi kirefu.
Awali inasemekana kuwa Askofu Mtega alipeleka ombi lake VATICAN kueleza kusudio lake la kutaka kustaafu kutokana na matatizo ya kiafya. Hata hivyo, ombi hilo lilichelewa kujibiwa hadi lilipojibiwa leo.
Norbert Wendelin Mtega (alizaliwa 17 Agosti 1945) eneo la Kinyika (Lupanga) Mkoani Njombe. Aliwekwa wakfu na Papa Yohane Paulo II mwaka 1986. Tangu mwaka wa 1992, amekuwa ni askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Songea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment