Marehemu
Gabriel Mwandemwa(Mwasyebule) enzi za uhai wake, Marehemu alikuwa
akijishughulisha na biashara mbali mbali ikiwemo uuzaji wa maziwa na
ununuzi wa mahindi.
MATUKIO
ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya
maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio la jana kijana wa
miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za kishirikina.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,
amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kumtaja marehemu liyetambulika
kwa jina la Gabriel Mwandemwa (Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande
Wilaya ya Rungwe aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu
vyenye ncha
kali sehemu za kichwani na kifuani.
Alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tano
asubuhi huko katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya
Busokelo, Wilaya ya Rungwe, mkoani hapa.
Alisema taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi
wa kimila kijijini hapo uliitisha kikao
cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji jirani na ndipo waliamua
kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria katika kikao hicho na kisha
kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni
mshirikina kijijini hapo kwa kuwa anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao
mengi kwa kuwatumikisha watu kishirikina.
Na Mbeya yetu Blog
Na Mbeya yetu Blog
0 comments:
Post a Comment