Kundi la wapiganaji wa
kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane
aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na
wanajeshi wa Marekani.
Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wanachama
wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo
,yapata kilomita 170 kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu .
Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab
limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar, katika mkutano uliofanyika katika
eneo lisilojulikana.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema kuwa kiongozi huyo hafahamiki vyema. BBC
0 comments:
Post a Comment