SIKU chache baada ya mwandishi wa habari, Dismas Lyassa kutangaza nia ya kuwania urais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), wajumbe wengine 40 wameelezwa kujitokeza kuwania nafasi hiyo.
Habari za ndani ya TUCTA ambazo Tanzania Daima
imezipata jana, kati ya hao 21 wametoka Chama cha Wafanyakazi wa Afya
na Serikali Kuu (TUGHE), na saba kutoka Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).
Pia kati ya wagombea hao, wanaotajwa kuwa na ushawishi mkubwa wa
kuukwaa urais ukiacha Lyassa ni Gratian Mukoba, ambaye kwa sasa ni Rais
wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).
Pamoja na kutojiweka wazi wakati wa kwenda kuchukua fomu za kuomba
ridhaa ya kuongoza shirikisho hilo ambalo linabeba dhamana ya
wafanyakazi takribani wote hapa nchini, orodha ya wajumbe ambayo
Tanzania Daima imeipata, inawajumuisha Odongo Silvery, Veronica Paulo,
Honest Temba, Amos Kabis, Optatus Silanda, Teresia Yomo, Charles
Kayombo, Notburga Maskini, Timotheo Kuchentama na Dk. Stephano
Chanangula wote kutoka TUGHE.
Wengine kutoka chama hicho ni Dk. Margreth Mtaki, Shaid Yusuph, Alois
Ngonyani, Raphael Mavunde, Rocky Malecela, Gresta Sodoka, Musiba
Kasoga, Dk. Idda Ngowi, Lydia Mhina, Bernard Mwingira na Andrew Kyando.
Kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU),
ni Sospeter Omollo, Alex Mkamba, Gerald Msanga, Crispin Kaijage, Frank
Chonya, Dinday Njile na Ally Mirambo wakati Chama cha Wafanyakazi wa
Bandari Tanzania (Dowuta), wamo Ajuaye Msese, Peter Bugingo na Liyasa
Kibeche.
Kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Mahotelini, Hifadhi na Majumbani
(Chodawu), waliojitosa ni Cosmas Chikoti, Muhsein Shariff na Sospeter
Kapanda wakati Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi (COTWU),
mbali na Lyassa, wamo Julius Rwabutomize na Juma Ng’imba huku CWT ni
Gratian Mukoba na Musa Mnyeti.
Pia vipo vyama ambavyo vimetoa mwakilishi mmoja kikiwemo Chama cha
Wafanyakazi wa Strabag (Tamico), kinachowakilishwa na Mbaraka Igangula
huku Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania
(Tewuta), kajitosa Jacob Nyajiego.
Tanzania Daima
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment