Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa madai ya kuasi dini ya kiislam ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa mara ya pili.
Meriam Ibrahimu alikwenda katika ubalozi wa Marekani uliyopo mji Mkuu wa Khartoum.
Mumewe ana asili ya Sudan Kusini lakini kwa sasa ni raia wa Marekani.
Mwanamke huyo aliachiliwa baada ya kuhukumiwa
adhabu ya kifo siku ya jumatatu lakini alishikiliwa tena na polisi kwa
tuhuma za kughudhi hati za kusafiria ili aondoke nchini Sudan kwenda
Marekani.
Kufuatia kuachiliwa huru kwa mara nyingine, Mke huyo wa Ibrahim ameiambia BBC kwamba ataendelea kuwa Mkristo.
Kesi yake ya kuasi dini imevuta hisia za watu wengi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu pamoja na nchi za Magharibi.
BBC
0 comments:
Post a Comment