Shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Kenya, NACADA, limeharamisha ladha kumi na tisa za Shisha.
Kwa mujibu wa afisaa mkuu mtendaji wa shirika
hilo Fazul Mohammed, shirika hilo kwa ushirikiano na wanasayansi wa
serikali waligundua kuwa ladha hizo wakati mwingi zinakuwa
zimechanganywa na madawa ya kulevya kama vile Cocaine na Heroine.
Utafiti wao waliufanya kisiri katika
mikahawa maarufu yenye kuuza Shisha na hapo ndipo waligundua kuwa
nyingi ya ladha za Shisha huwa zimechanganywa na madawa ya kulevya.
Baadhi ya ladha hizo pia ziligunduliwa kuwa na Bhangi.
Akiongea na BBC bwana Fazul alisema kuwa shirika
hilo linatafakari kupiga marufuku Shisha kwa sababu ya madhara yake kwa
afya ya watumiaji na hasa kwa kuwa nyingi zinachanganywa na madawa ya
kulevya.
Ladha hizo ambazo zinapaswa kuondoshwa sokoni
mara moja ni pamoja na Al Fakher yenye ladha ya strawberry , Al Fakher
yenye ladha ya chungwa , Al Fakher yenye ladha ya tufaha, Al Fakher
vanilla , Al Fakher Mapera, Al Fakher appeals, Al Fakhar chungwa ikiwa
na ladha ya mint na nyinginezo.
Kwa mujibu wa Bwana Fazul, kwa wale watakoapatikana wakitumia Shisha lenye ladha hizo ambazo zimepigwa marufuku, watashitakiwa.
Mwenyekiti wa tume ya shirika hilo, John
Mututho, amenukuliwa akisema watakaopatikana wakiuza au kutumia bidhaa
hizo, watafikishwa mahakamani.
BBC
0 comments:
Post a Comment