Shambulio limetokea katika jimbo la Yobe nchini Nigeria wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia.
Jimbo hilo limewekwa katika hali ya hatari huku
maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio yanayofanywa na
wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wakaazi wanasema walisikia sauti ya
mlipuko mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu ambapo
mashabiki wa soka walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe la dunia.
Walioshuhudia wanasema mshambuliaji wa kujitolea
mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na mgahawa
katika jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.
Duru kutoka hospitalini zinasema malori kadhaa
yamewasafirisha majeruhi kupata matibabu na polisi wanasema maafisa
wamepelekwa katika eneo hilo.
Mfanyakazi mmoja wa hospitali ameaimbia BBC kuwa
waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu
na mikono.
Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo
la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria
walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za
kombe la dunia kutokana na hofu ya Usalama.
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.
'Hali ya hatari'
Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika
hali ya tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila
mara ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009.
BBC
0 comments:
Post a Comment