Shughuli katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Jomo Kenyatta zilisitishwa kwa muda Jumatano asubuhi
baada ya mwili wa kijana mdogo kupatikana karibu na eneo la kurukia
ndege.
Mkuu wa kitengo cha Polisi katika uwanja huo,
kamanda, Joseph ole Tito, amesema kuwa mwili huo ulipatikana katika
sehemu ya kurukia ndege
Hata hivyo alisisitiza kuwa ndege zilizokuwa zinaingia uwanjani humo asubuhi na mapema hazikuathiriwa na tukio hilo.
Halmashauri ya huduma za ndege ilisema kuwa uwanja ulifungwa kwa dakika arobaini baada ya maafisa wa usalama kugundua mwili huo.
Kwa mujibu wa maafisa hao, hatua ya kufunga uwanja huo ilifanywa ili kuondoa mwili wa kijana huyo
Ni ndege ya shirika la ndege la Uturuki tu ndiyo
ililazimika kusalia angani kwa muda huku mwili wa kijana huyo
ukiondolewa uwanjani.
Kijana huyo anaaminika kuwa na kati ya umri wa miaka 10 na 12 na alikuwa na majeraha upande wa kushoto wa mwili wake.
''Mwili wake uliondolewa katika eneo hilo na kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa,'' alisema bwana Tito.
Polisi wamesema watafanya uchunguzi kubaini
ikiwa alianguka kutoka kwenye gurudumu la ndege au mtoto huyo alifariki
kutokana na sababu nyinginezo.
Pia miongoni mwa maswali yanayoulizwa ni vipi mwili wake ulipatikana katika uwanja wa ndege hasa katika njia ya kurukia ndege?
Visa vya watu kupanda kwenye magurudumu ya ndege
kimagendo kwa lengo la kusafiri kwenda nchi nyingine vimekuwa
vikiripotiwa hivi karibuni.
BBC
0 comments:
Post a Comment