Viongozi wa Matawi ya Yanga wakiongozwa na Mohamed Msumi (wa kwanza
kulia) wameutaka uongozi kuwachukulia hatua wanachama na viongozi
wa Matawi wanaochochea vurugu katika klabu hiyo kwa mujibu wa katiba na
miongozo ya klabu hiyo.
Pia wamewaonya baadhi ya wanachama ambao wamekuwa
wakiongelea masuala ya klabu hasa ya kiutawala pasipo kupata ruhusa ya
mwenyekiti na kuchafua hali ya hewa ndani ya klabu hiyo kuacha mara moja
vinginevyo watachukuliwa hatua kwani kanuni zipo wazi kwa sababu
wanatakiwa kutoa maoni yao kupitia mkutano mkuu na vikao halali ama kwa
ruhusa ya mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji.
Baadhi ya wanachama wamekuwa wakipinga maamuzi
yaliyipitishwa na klabu hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika mwanzoni
mwa mwezi huu wa kumuongezea mwaka mmoja Yusufu Manji ili aweze
kutekeleza malengo aliyojiwekea kitendo kinachodaiwa kwenda kinyume cha
katiba ya klabu ya Yanga .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment