Kiongozi wa zamani wa waasi katika Jamhuri ya
kidemokrasia ya Bosco Ntagandaa amefikishwa katika mahakama ya
kimataifa ya makosa ya jinai ICC huko The Hague.
Mwendesha mkuu wa mashitaka ICC,Fatou Bensouda amesema kuwa Ntaganda aliamuru watu kuwaua na kuwabaka waathiriwa wa vita.
Bensouda pia alisema kuwa Bosco
alihusika pakubwa katika kupanga mashambulizi dhidi ya raia. Kadhalika
aliongeza kuwa Ntaganda aliwahukumu watu kwa msingi ya kabila lao kwa
kuwafukuza, kuwaua, kuamuru wabakwe na kuwatumia kama watumwa wa ngono.
Hata hivyo Generali Ntanganda amekanusha
kuhusika na makosa ya kivita katika maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo
miaka kumi iliyopita.
Bosco Ntaganda, anayefahamika sana Nchini
Congo kwa jina Terminator yuko mahakamani kama mshukiwa wa kwanza kuwahi
kujisalimisha mwenyewe.
Alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani Nchini Rwanda mwaka jana.
Bwana Ntaganda ambaye ni mshukiwa aliyekuwa
akisakwa zaidi na ICC anatuhumiwa kutekeleza makosa 18 ikiwemo kuwatumia
wasichana kama wafungwa wa ngono.
Majaji katika kesi hiyo wataamua kama Ntaganda ana kesi ya kujibu au la.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment