
Uharibifu wa Boko Haram
Maafisa katika eneo la kaskazini
mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa zaidi ya watu mia mmoja wameuwawa
katika shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislamu wa
Boko Haram.
Shambulizi hilo katika kijiji cha Izghe katika
jimbo la Borno linajiri siku nne pekee baada ya watu 39 kuuwawa katika
shambulizi jingine.
Seneta
wa jimbo la Borno Mohammed Ali Ndume ameiambia BBC kwamba watu mia moja
na sita waliuwawa katika shambulizi hilo la hivi punde.
Amesema takriban wanamgambo mia moja walivamia
mji wa Izghe jumamosi usiku. Wananchi waliokuwa wakikimbia mashambulizi
hayo wamethibitisha kuwa takriban wanaume thelathini walikusanywa na
kisha kupigwa risasi.

Wanamgambo wa Boko Haram
" Waasi hao walikuja karibu saa tatu usiku na
kisha kuwakusanya wanakijiji katika makundi, hususan vijana. Kisha
wakaenda nyumba hadi nyumba na kuwauwa wanaume, na kuchukuwa kila kitu
walichokuwa nacho,'' amesema Ali Ndume.
"Wamewauwa watu 106 ambapo 105 kati yao ni
wanaume na mwanamke mmoja kikongwe ambaye alikuwa akijaribu kumlinda mjukuu
wake wa kiume asiuawe. Nadhani alipigwa risasi na kisha akafa."
Baada ya hapo wanamgambo hao walienda nyumba hadi nyumba
wakiwauwa watu ambapo wengi wao wakiwa ni wanaume. Baadhi walipigwa risasi
huku wengine wakichinjwa.
Msemaji wa jeshi hakutoa maelezo kuhusu kisa
hicho cha hivi punde lakini ameiambia BBC kwamba jeshi haliwezi kuwa
kila mahali na kusema kuwa wanamgambo hao ni watu wa kuhamahama.
0 comments:
Post a Comment