Ndege iliyotekwa
Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia ndiye aliyeiteka nyara .

Maafisa mini Geneva wanasema kuwa msaidizi huyo wa rubani alichukua usukani wa ndege hiyo rubani wake alipokwenda msalani kwa haja.

Tukio hilo linaripotiwa kutokea ndege hiyo aina ya Boeing 767-300 ilipokuwa ikipaa katika anga ya Sudan.

Rubani huyo msaidizi alibadili uelekeo wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Rome Italia,na kuipaisha hadi Uswisi alipoitua katika uwanja wa ndege wa Geneva.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote 200 wako salama .

Ripoti ya idara inayosimamia usafiri wa ndege ya Uswisi inasema kuwa rubani huyo msaidizi aliomba uraiya kabla ya kutua ndege hiyo na akajisalimisha kwa maafisa wa usalama waliokuwa wameizingira ndege hiyo.

Polisi walimtia mbaroni mara moja .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top