Victoire Ingabire akiwa mahakamani 
Mahakama ya juu zaidi nchini Rwanda imeendeleza hukumu ya kwanza aliyopewa kiongozi wa upinzani nchini humo Victoire Ingabire na kuiongeza kutoka miaka 8 hadi 15.

Awali mwezi Oktoba, bi Ingabire ambaye ni wa asili ya ki Hutu alipatikana na hatia ya ugaidi, na kukana kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya kabila la wa Tutsi.

Mauaji hayo yalifanyika mwaka 94 ambapo zaidi ya watu 800 wa kabila la wa Tutsi waliuawa.

Bi Ingabire alikata rufaa dhidi ya hukumu ya awali aliyopewa japo upande wa mashtaka nao ulitaka aongezewe hukumu hiyo na hata kupendekeza apewe hukumu ya maisha gerezani.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeshutumu namna kesi ya Bi Ingabire imeendeshwa.

Bi Ingabire amekumbwa na matatizo na sheria ya Rwanda baada ya kurejea nchini humo mwaka wa 2009, kutoka Uholanzi alikoishi kwa miaka kadhaa. Alieleza wazi nia yake kuwania urais nchini humo lakini hakupata fursa kwani punde tu alipowasili alifunguliwa mashtaka hayo.

Kutokana na kujivuta kwa kesi yake, hakushiriki uchaguzi uliofuata wa mwaka wa 2010. Tangu wakati huo, amekuwa kizuizini. Amekuwa akiwakilishwa na wakili kutoka Uingereza.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top