Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Wamiliki wa makampuni ya nje yanayoendesha shughuli
katika baadhi ya sekta nchini Zimbabwe kuanzia Januari mosi mwaka 2014
hawataruhusiwa na iwapo watakiuka agizo hilo watakamatwa mmoja wa
maafisa waandamizi wa serikali ya nchi hiyo amesema.
Katibu wa Uwezeshaji Uchumi George Magosvongwe alitoa onyo katika bunge la nchi hiyo, gazeti moja la serikali limesema.
Kumilikisha uchumi kwa wanyonge ni moja ya kampeni ya Rais Robert Mugabe katika uchaguzi uliofanyika mwezi Machi.
Kilimo, maduka ya kunyoa nywele, biashara za
saluni, biashara ya kuuza vitafunio ni miongoni mwa kazi zitakazofanywa
na wazawa pekee nchini humo.
"Kuanzia Januari mosi mwezi mmoja unaokuja
tutaanza kuchukua hatua na tayari tumeandaa utaratibu na hatua za
kuchukuka kwa wal watakaokiuka agizo hilo," Gazeti la serikali ya Herald
limemnukuu Bwana Magosvongwe akisema.
Amesema raia wa Zimbabwe wamekwishaandaliwa ili
kuchukua nafasi za kuendesha shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na wageni
ili kuepuka upungufu wa bidhaa.
Kwa mujibu wa gazeti la Herald biashara
zilitengwa kwa wazawa ni pamoja na biashara za reja reja na jumla,
maduka ya kunyoa, biashara za saluni, biashara za kutengeneza na kuuza
vitafunio, kilimo , usafirishaji, biashara za majengo na matangazo.
Amesema migahawa inayomilikiwa na wageni ambayo haitengenezi vyakula vya asili haitaathirika.
Wamiliki wa biashara ambao hawatakidhi vigezo
vya biashara za wazawa watakuwa katika hatari ya kupigwa faini au
kifungo kama wataendelea kufanya biashara hizo gazeti la Herald
limesema.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment