Tunawashukuru watanzania kwa
kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa
na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo.
Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na
kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za
mabadiliko.
Haya ni mawimbi katika harakati za
mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika
mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu.
Ninashauri tuwe na subira katika kutoa
hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata
upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo
mpitishe hukumu.
Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa
habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na
hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni
wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu.
Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi
bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia
kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa
nchini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment