Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,Joseph
Kabila, anatembelea eneo la mashariki mwa Congo ambalo awali
lilidhibitiwa na kikundi cha waasi wa M23, ambacho kilishindwa katika
mapigano dhidi ya majeshi ya Congo yakisaidiwa na yale ya Umoja wa
Mataifa, mwezi mmoja uliopita.
Anatarajiwa kuwasili eneo la Rutshuru -- eneo ambalo lilikuwa ngome kuu ya waasi karibu na mpaka wa Uganda.
Bwana Kabila amefanya safari ya urefu wa
kilomita mia tisa kwa njia ya gari mashariki mwa Congo kuonyesha imani
yake kuhusu kuimarika kwa usalama katika eneo hilo.
Amevitaka vikundi vingine vyenye silaha nchini
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kujisalimisha, la sivyo vitashughulikiwa
kama ilivyotokea kwa kikundi cha M23.
Eneo la Rutshuru lilikuwa chini ya udhibiti wa
M23 kwa zaidi ya mwaka mmoja na wakaazi wa eneo hilo wameiambia BBC kuwa
waasi hao waliwaua na kuwateka watu wengi.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment