Makaduka yakiwa yamefungwa katika Mtaa wa Kongo jijini Dar es Salaama
jana kutokana na wafanyabiasha kugoma ili kushinikiza Mamlaka ya
Mapato kusitisha matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti
(EFD
Wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam jana walifunga
maduka yao kupinga utaratibu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
wa kutoza kodi kwa kutumia mashine za elektroniki (EFD).
Wafanyabiashara walifanya mgomo huo ili
kushinikiza kuonana na ama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha,
Dk William Mgimwa au Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Wanadai kuwa mashine hizo za EFD zinauzwa bei
ghali ya kati ya Sh800,000 hadi Sh1.2 milioni, gharama ya kuzifanyia
matengenezo zinapopata hitilafu ni kubwa na pia wanadai kuwa kuna harufu
wa ufisadi kwenye suala hizo kwa kuwa ni kampuni chache zilizochaguliwa
kuuza mashine hizo.
Maduka karibu yote hayakufunguliwa tangu alfajiri
tofauti na ilivyozoeleka na hata wafanyabiashara wachache waliojaribu
kufanya hivyo walilazimika kuyafunga kwa hofu ya kufanyiwa vurugu na
wenzao.
Baadhi ya maduka ya vifaa vya umeme, magodoro na
friji yaliyopo Mtaa wa Uhuru yalikuwa wazi lakini baada ya muda mfupi
yalifungwa.
Hata hivyo, maduka yaliyoko kwenye Soko Kuu la Kariakoo yalikuwa wazi muda wote.
Mgomo huo ulianza baada ya wafanyabiashara hao
kupeana taarifa wakihamasishana kutokufungua maduka yao kushinikiza
kusikitishwa kwa matumizi ya mashine hizo za kukokotoa kodi.
Msimamo wa Serikali
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema mgomo
wa wafanyabiashara wa Kariakoo hauwezi kubadili msimamo wa Serikali wa
kukusanya kodi kwa kutumia mashine za EFD. Alisema suala la bei haliwezi
kuwa kigezo cha kugoma kwa kuwa baada ya kununua fedha zao zitarejeshwa
kidogokidogo kwenye marejesho ya kodi.
“Changamoto iliyopo ni kwamba wafanyabiashara
wengi hawajui kama fedha hizo wanazonunulia mashine watarejeshewa kwenye
makato ya kodi. Hatuwezi kuzibadilisha mashine hizo kwa kuwa siyo kama
simu za mkononi, zimetengenezwa kwa mfumo maalumu wa TRA,” alisema.
Aliitaka TRA kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu manufaa ya kutumia mashine hizo.
TRA yakaza uzi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa
TRA, Richard Kayombo aliwataka wafanyabiashara kuacha kutafuta mbinu za
kukwepa kulipa kodi na badala yake wawe wazalendo kwa nchi yao.
“Unajua wafanyabiashara wengi wanaumia kulipa
kodi, sasa wanatafuta visingizio na kufanya mbinu chafu ili kukwepa.
Mbinu zao tumezigundua kwani kuna baadhi yao wanadiriki hata kusema hata
wakipewa bure mashine hizo watazichoma moto,” alisema Kayombo.
Alisema madai ya wafanyabiashara hao kwamba kuna upendeleo katika kutoa zabuni ya kuuza mashine hayana ukweli wowote na kusema kampuni kumi na moja zimepewa zabuni ya kuuza mashine hizo baada ya kushinda mchakato ambao ulitangazwa kwa kufuata vigezo vyote.
Alisema madai ya wafanyabiashara hao kwamba kuna upendeleo katika kutoa zabuni ya kuuza mashine hayana ukweli wowote na kusema kampuni kumi na moja zimepewa zabuni ya kuuza mashine hizo baada ya kushinda mchakato ambao ulitangazwa kwa kufuata vigezo vyote.
Kuhusu suala la bei ambalo wafanyabiashara
wanasema mashine hizo zinauzwa bei kubwa ya Sh800,000. Kayombo alisema:
“Tumeliona hilo na baada ya majadiliano tumepunguza bei ya mashine hizo
na sasa zinauzwa Sh600,000.”
Madai mengine ya wafanyabiashara kwamba mashine
hizo zinatoa majibu tofauti, Kayombo aliwataka wanaopata tatizo hilo
kutoa taarifa sehemu inayohusika kwa utatuzi.
“Hebu nikuulize ndugu yangu, hivi kama nyumbani
kwako umeweka umeme, ukaamka siku moja na kukuta luku haifanyi kazi,
utagoma au utatoa taarifa kwa mamlaka husika?
Msimamo wa wafanyabiashara wa Kariakoo
Mshauri wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Karikaoo
(JWK), Johnson Minja alisema wanataka kuzungumza na Serikali ili kupata
mwafaka wa suala hilo.
“Wafanyabiashara wana malalamiko mengi siyo suala
la kuanzishwa kwa mfumo wa mpya wa elektroniki pekee, bali pia wamegoma
kutokana na kero mbalimbali zinazolikabili eneo hili,” alisema Minja.
“Tuliandika barua kwenda Wizara ya Viwanda na
Biashara tukimtaka Waziri husika kuonana naye na kujadili juu ya kuwepo
kwa kero mbalimbali kama kukithiri kwa wamachinga, uchafu na jinsi ya
kutumia hizi mashine mpya za kielektroniki lakini hatujapata majibu,”
alisema Minja.
Mmiliki wa maduka ya magauni ya madera, Mwinyihaji
Hussein alisema wataendelea na mgomo hadi pale Serikali itakapoona kuna
haja ya kukutana nao na kuzungumzia suala hilo akidai kwamba kuna
harufu ya ufisadi ndani yake.
“Kwa bei ambazo mashine hizo zinauzwa unafikiri ni
wafanyabiashara wangapi ambao watamudu kuzinunua?... maduka yatabaki
yamefungwa hadi kieleweke,” alisema. Mfanyabiashara wa vifaa vya umeme,
Jedda Hasabubaba alisema wanaitaka Serikali kuchaji kodi hiyo ya VAT
bandarini na si katika maduka.
“Ule utaratibu wa mwanzo, TRA ilikuwa inavuka
lengo katika kukusanya mapato kwa nini tusiendelee na mfumo huo badala
ya kutumia hizi mashine za kielektroniki?
Morogoro
Mgomo huo wa wafanyabiashara wa Kariakoo umekuja baada ya wenzao wa Morogoro kufanya hivyo kwa madai yanayofanana.
Hata hivyo, walisitisha mgomo huo kwa muda kuipa
nafasi Serikali kushughulikia kero zao ambazo ni kupunguza gharama ya
kununua mashine hizo na tozo ya kodi ya asilimia 18.
Mwananchi
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment