Majeshi ya Marekani yanayoshauri wanajeshi wa Uganda katika msako dhidi ya Kony.
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati inasema inajadiliana na kiongozi aliyetoroka wa waasi kutoka Uganda Joseph Kony.
Msemaji wa serikali ameiambia BBC kwamba Joseph
Kony alikuwa katika Jamhuri ya Afrika ya kati, lakini alitaka
kuhakikishiwa usalama wake kabla hajajisalimisha.
Marekani imekuwa ikivisaidia vikosi vya Uganda kumsaka Kony anayeongoza kundi la waasi la LRA, na anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Marekani ilikuwa imeahidi kumtuza dola milioni 3.3 yeyote mwenye taarifa itakayopelekea kukamatwa kwa Kony
Hii ni mara ya kwanza kwa miaka mingi, kwa taarifa kuhusu aliko Kony kutolewa.
Pia mnamo siku ya Jumatano, mjumbe maalum wa
muungano wa Afrika kuhusu LRA, Francisco Madeira, aliambia baraza la
usalama la umoja wa mataifa, kuwa aliona ripoti kuwa Kony anaugua
ugonjwa mbaya sana usiojulikana.
Mnamo mwezi Aprili, jeshi la Uganda lilisitisha
msako dhidi ya Kony katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, likisema kuwa
linabiliwa na mashambulizi makali kutoka kwa serikali waasi
walipochukua mamlaka baada ya mapinduzi.
Joseph Kony pamoja na wapiganaji wake walio kati
ya 200-500, wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Uganda kwa zaidi
ya miaka 20.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment