Chama cha Wananchi (CUF), kimeanza harakati za kuelekea kushika dola mwaka 2015 kwa kutangaza kuanza chaguzi ndani ya chama hicho kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa Chama hicho, Shaweji Mketo akizumgumza jana alisema, uchaguzi huo una lengo la kuwapata viongozi wapya watakaokiongoza kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Mketo akitangaza ratiba ya uchaguzi huo alisema, uchaguzi wa Ngazi ya Taifa utafanyika Mei 6 hadi 31 mwaka 2014, ambapo fomu zitaanza kutolewa Machi 28 hadi Aprili 10 mwaka 2014.
Alisema Ngazi ya Matawi, uchukuaji wa fomu umeanza jana Novemba 1 mwaka huu, na uchaguzi wake utafanyika Novemba 11 hadi 30 mwaka huu.
“Ngazi ya Kata fomu zitaanza kutolewa Desemba Mosi hadi 10 mwaka huu na uchaguzi wake utafanyika Januari Mosi hadi 10 mwakani,” alisema Mketo.
Mwananchi 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top