Silvio Berlusconi
Bunge la Seneti nchini Italia limepitisha hoja ya
kumtimua Waziri Mkuu mstaafu wa Italia Silvio Berlusconi katika bunge
kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi.
Kufuatia hatua hiyo sasa Berlusconi anaweza kushtakiwa kutokana na kukosa kinga ya bunge.
Kwa upande Berlusconi amewaambia
wafuasi wake kuwa leo ni siku ya maombolezo katika demokrasia na kwamba
kura hiyo ya bunge la seneti inaonyesha chuki binafsi ya wale wa upande
wa kushoto.
Berlusconi alijiondoa siku ya jumanne katika
chama cha Forza Italia ambacho kipo ndani ya serikali ya mseto
inayotawala nchi hiyo, hata hivyo serikali iliepuka kura ya kutokuwa na
imani na kufanikiwa kupitisha bajeti.
Mjadala katika bunge la seneti umekuwa mkali ambapo maseneta kutoka pande zinazopingana wamekuwa wakitupiana maneno makali.
Manuela Ripetti kutoka chama cha Berlusconi cha
Forza Italia alisikika akipaza sauti "Tunajua nia yenu ni kumwondoa
Silvio Berlusconi".
Awali Berlusconi ambaye ametawala katika siasa
kwa miongo miwili nchini Italia amewaomba maseneta kusogeza mbele kura
hiyo ya kumwondoa kwa madai kwamba anao ushahidi unaothibitisha kuwa
hajafanya kosa la kukwepa kodi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment