Serikali ya Misri imechukua hatua ya kupiga tanji na
kuchukua mali ya vuguvugu la Muslim Brotherhood baada ya harakati za
kundi hilo kuharamishwa kufuatia msako mkubwa uliofanywa na serikali.
Imesema kuwa itaharamisha au kuchukua usimamizi
wa huduma ambazo zilikuwa zinatolewa na vuguvugu hilo ikiwemo za
hospitali, shule na huduma nyingine za kijamii.
Hatua ya serikali ya kuharamisha
shughuli za kundi hilo ilikuja baada ya mahakama kuamua hivyo lakini
imethibitishwa kutokana na rufaa za chama hicho.
"Kulingana na sheria, msitari wa mwisho unasema sasa wameharamishwa,” alisma afisaa mmoja wa serikali.
Kwa mujibu wa msemaji wa waziri wa maswala ya
kijamii, ambaye ndiye alichukua hatua ya kuharamisha vuguvugu hilo,
baraza la mawaziri liliafikiana kuunda kamati kuchunguza chanzo cha
ufadhili wa vuguvugu hilo na kutaifisha mali zake.
Alisema kuwa ikiwa mipango ya chama hicho
itagundulika kuwa na uhusiaono wowote na vuguvugu la Muslim Brotherhood –
iwe ya elimu au kiafya , basi uamuzi utafanywa na mahakama na serikali
kuzisimamia.
'Kuwajibishwa’
Kipindi cha siku 15 cha kukata rufaa dhidi ya
hatua ya mahakama kinakwisha Jumatatu , lakini hatua zilichukulilwa
mapema ili mawaziri wajizuie kukutana kwa siku tatu zijazo ambazo ni
siku za mapumziko.
Muslim Brotherhood waliingia mamlakani miezi 14
iliyopita lakini jeshi likamwondoa mamlakani aliyekuwa rais, Mohammed
Morsi, na hajaonekana hadharani, tangu mwezi Julai kufuatia maandamano
makubwa dhidi ya utawala wake.
Wengi wa viongozi wa vuguvugu hilo wako jela na linasema kuwa wafuasi wake wengi wameuawa katika misako ya polisi na jeshi.
Licha ya hatua ya serikali kuharamisha chama,
wafuasi wa Brotherhood wanaendelea kujitokeza barabarani kuandamana
ingawa idadi yao ni ndogo sana ikilinganishwa na siku za nyuma.
Chama ambacho kimekuwa kikikandamizwa kwa miaka
mingi , sasa kwa mara nyingine kinalazimishwa kujiondoa kutoka ulingo wa
siasa , lakini bila shaka kitasalia kuwepo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment