Rais Bashar al Assad
Rais wa Syria Bashar al-Assad amepongezwa na Marekani
kwa kutii na kutekeleza azimio la UN na kukubali kuharibi silaha za
kemikali zilizotumiwa kuwaua mamia ya watu nchini Syria mwezi Agosti.
Pongezi hizi zimetolewa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry.
Kerry alikuwa anazungumza baada ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kusema kuwa silaha hizo tayari zimeanza kuharibiwa.
Juhudi za kuharibu silaha hizo ziliafikiwa
katika azimio la UN ambalo lilipitishwa baada ya makubaliano kati ya
Urusi na Marekani.
Azimio hilo nalo lilikuja baada ya dunia nzima
kulaani matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya raia katika kitongoji
kimoja karibu na mji wa Damascus.
Marekani hata hivyo ilikuwa imesisitiza kuwa
lazima Serikali ya Syria iadhibiwe kijeshi kwa kutumia silaha za
kemikali dhidi ya raia wasio na hatia.
Hata hivyo serikali ya Bashar al Assad ilisisitiza kuwa haikutumia silaha hizo na kudai waasi ndio waliozitumia dhidi ya raia.
Madai ambayo yalipingwa vikali na serikali ya Syria na hata kuungwa mkono na Urusi.
Azimio la kuitaka Syria kuharibu silaha hizo
liliafikiwa mwezi jana baada ya muda mrefu wa mvutano hulihusu katika
Umoja wa Mataifa baadhi ya nchi zikitaka kipengee cha kuadhibu Syria
kijeshi ikiwa itakataa kutii matakwa ya UN kuondolewa kwenye azimio
hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment