Rais Francois Hollande anasema Syria lazima ishinikizwe
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja
makubaliano kati ya Marekani na Urusi kuhusu silaha za kemikali za Syria
kama hatua muhimu katika suluhu kubwa zaidi la mgogoro wa kisiasa
unaokumba taifa hilo.
Lakini kwenye hotuba yake bwana Hollande
aliongeza kusema kuwa "lazima wazo la kuchukulia Syria hatua za kijeshi
lisalie , la sivyo hapatakuwa na shinikizo.’’
Aidha Bwana Hollande alisema huenda
nchi wanachama wa baraza hilo wakakubaliana kuhusu kura katika baraza la
usalama la umoja wa Mataifa kwa azimio kuhusu Syria.
Holland anatarajiwa kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry hii leo kujadili swala hilo.
Rais huyo amesema kuwa sharti Syria iwekewe
vikwazo ili iharibu silaha zake za kemikali ikiwa itakataa kufuata
maagizo na matakwa ya mataifa ya nchi za kigeni.
"Ni muhimu kuongeza kwa haya yote tisho la
kuiwekea Syria vikwazo ikiwa makubaliano na malengo ya baraza la usalama
ya Umoja wa Mataifa hayatatimizwa,’’ aliongeza kusema Rais Hollande
"Lakini hatua inayofuata ni kutafuta suluhu la kisiasa kwa haya yote.’’
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment