Ruto akiwa na Joshua Arap Sang wakati kesi dhidi yao ilipowasilishwa katika mahakama ya ICC
Kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto, imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague.
Bwana Ruto anayetuhumiwa kwa kuchochea ghasia za
baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007, alikana mashtaka yote dhidi yake.
Vile vile mshtakiwa mwenza mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang pia
alikana mashtaka.
Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kuhusika na ghasia hizo anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba.
......Ikiwa unafuatilia kesi hiyo unaweza kutupa maoni yako kuhusu inavyoendeshwa kwenye ukurasa wetu Bofya
facebook Bofya
bbcswahili kisha tutayaweka maoni yako hapa.......
12:24 PM: Wakili Stenberg
ambaye anaendelea kuelezea mahakama kuhusu ushahidi wao amesema kuwa
Ruto alisambaza silaha kwa vijana ambao wangefanya mashambulizi dhidi ya
watu wa kabila hasimu waliokuwa wanaishi katika mkoa wa Rift Valley
12:13 PM Wakili Steynberg wa
upande wa mashtaka amesema kuwa Ruto aliahidi kuwazawadi wale ambao
wangefanya uhalifu katika mikutano ambayo vijana walihudhuria kwa wengi
wakati wakipangia vurugu baada ya uchaguzi
12:01PM Upande
wa mashtaka unasimulia ambavyo unapanga kuthibitisha kuwa kesi yao ni
ya uhakika, ushahidi utakaotolewa , na nani atakayetoa ushahidi huo.
Mashahidi inasemekana watawataja wahusika wengine kwenye kesi hiyo hasa
walioshirkiana na washtakiwa kufanikisha mipango yao.
11:55AM:
Upande wa mashtaka kupitia kwa wakili Steynberg umeiambia mahakama kuwa
kila mshukiwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuwalazimisha watu
kuondoka makwao kwa lazima, mauaji na kuchochea ghasia
11:51AM:
Bensouda aambia mahakama kuwa amekuwa na wakati mgumu sana kukusanya
ushahidi wa kesi yake akisema kuwa wengi wa mashahidi wamejiondoa katika
kesi hiyo wakisema wanahofia maisha yao na kuongeza kuwa baadhi pia
wamehongwa ili wasitoe ushahidi wao.
11:41 AM: Fatou Bensuda
mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama hiyo aelezea mahakama kuhusu
tuhuma zinazowakabili Ruto na Sang kwa kuchochea ghasia za baada ya
uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008. Bansuda amesema kuwa Ruto alifanya mauaji
kwa sababu za kisiasa huku Sang akimsaidia kuchochea ghasia ili
kumsaidia kufanikisha ajenda yake ya kuingia mamlakani
11:35AM Joshua Sang pia amekanusha mashtaka yote dhidi yake
11:33 AM Ruto amekana mashtaka
yote aliyosomewa na upande wa mashtaka kuwa alihusika na uhalifu dhidi
ya binadamu , mauaji, dhulma na kuwaondosha watu makwao kwa lazima
11:24: AM Naye
Joshua alisomewa mashtaka dhidi yake ya kuchochea ghasia katika mkoa wa
Rift Valley kwa kutumia kituo cha redio alichokuwa anafanyia kazi
kueneza chuki na ukabila
11:23 AM Ruto asomewa mashtaka dhidi yake na kuambiwa kuwa alihusika na mauaji ya watu katika mkoa wa Rift Valley
11:20AM :Kesi
dhidi ya mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya
Naibu Rais William Ruto imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa
ya ICC .
11:00AM:
Wahusika wote kwenye kesi hii kutoka upande wa naibu rais Ruto, mshukiwa
mwengine Joshua Arap Sang na upande wa mashtaka wake Fatou Bensauda
walijitambulisha mahakamani kwa ombi la mmoja wa majaji kwenye jopo la
majaji
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment