Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi
ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Ofisi ya CCM Tawi
la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza
namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi
wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara.
Katibu Mkuu wa
CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa
Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo
yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya
hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao
wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya
Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na
kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa
serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo
Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na
kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza
vikundi.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
wakiongea na wananchi wa Nyamongo ,Wananchi wa Nyamongo wameshukuru sana
kwa kusikilizwa kwa ukaribu haijawahi tokea na wameahidi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Viongozi hao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo.
Sehemu ya wakazi
wa Nyamongo wakiwa kwenye kikao cha ndani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye,Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele na Viongozi
wengine wa Serikali ambapo walikaa na kujadili matatizo yao namna ya
kuyatatua.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ,leo amefanya ziara katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara .
Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele alilazimika kupangua ratiba ya ziara baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.
Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.
- Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo.
- Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.
- Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali , chama na wananchi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment