Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto
Kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto itaanza hii leo katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC , Hague Uholanzi.
Bwana Ruto na Rais Uhuru Kenyatta, wanatuhumiwa
kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 - madai
anayoyakanusha.
Majaji wa mahakama hiyo wameelezea
kuwa kesi hizo mbili huenda zikafanyika wakati tofauti katika kipindi
chja wiki nne kila mmoja wala sio kwa wakati mmoja kama ilivyokuwa
imepangwa zisikilizwe kwa wakati mmoja.
Hii ni kutokana na ombi la rais Kenyatta kuwa
washukiwa hao hawapaswi kuwa nje ya nchi kwa wakati mmoja kwani kutakuwa
na pengo la uongozi.
Duru zinasema kuwa hii bila shaka ndiyo kesi yenye utata mkubwa zaidi kuwahi kusikilizwa katika historia ya mahakama ya ICC.
Kesi ya Kenyatta inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Novemba.
Ghasia hizo ambazo zilizuka baada ya aliyekuwa
Waziri Mkuu Raila Odinga kupinga ushindi wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki,
watu 1,300 walifariki.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment