Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda
yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao
walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya
ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na
hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari
ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa
watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo alifariki kutokana na
majeraha yake.
Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana
mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na
shughuli zao zakawaida.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
2 comments:
Pole sana wa Kenya kwa kitondo kilicho tendeka uko, hivi kwa nini maduka kama hayo akuna ulinzi mkali.
poleni wakenya na nimefurai kwa kuwazibiti hao magaidi
Post a Comment