Raia wa Australia wamemaliza kupiga kura katika
uchaguzi mkuu ambapo waziri mkuu wa chama cha Labor, Kevin Rudd,
anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Tonny Abbott.
Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha Bwana
Abbot na chama chake cha Liberal-National akiongoza, lakini wanasiasa
wote wawili wanasema matokeo hayatabiriki na waliwaomba wafuasi wao
wapige kura.
Foleni zilikuwa ndefu katika vituo vya kupiga
kura - katika sheria ya Australia kupiga kura ni lazima kwa kila mtu
zaidi ya umri wa miaka 18.
Maswala muhimu katika kampeni yalikuwa uchumi, wahamiaji na kodi juu ya uchafuzi wa mazingira.
Lakini katika kampeni wanasiasa wenyewe ndio walikuwa muhimu kushinda mjadala.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment