Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali wametakiwa kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa na wahisani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

Hayo yamesemwa na afisa mawasiliano wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Rebeka Kwandu wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa kuendeleza miji hapa nchini.

Afisa huyo amekiri kuwepo kwa ubadhirifu katika halmshauri mbalimbali hapa nchini ambapo katika mwaka 2009 -2012 jumla ya wakurugenzi 24 na watendaji wengine wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria.

Afisa huyo amesema kuwa miji saba imetengewa dola za marekani milioni 175 kutoka Benki ya Dunia na Shirika la Misaada la Denmark (DANIDA).

Katika hatua za awali mikoa ambayo inataraji kuendelezwa kutokana na fedha hizo ni pamoja na Mbeya, Dodoma, Arusha, Kigoma, Mtwara, Tanga na Mwanza.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top