Prof. Sospeter Muhongo
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema takwimu zinonesha kuwa kwa sasa hamna bwawa lolote la maji ya kuzalisha umeme ambalo lina maji  ya kuzalisha umeme wa kutosha hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa  jijini Dar es Salaam alipoulizwa ni kwanini Serikali haikutaka kutumia Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) ili kuzalisha umeme pamoja na kwamba tafiti zinaonesha kuwa lingeweza kuzalisha umeme wa zaidi ya megawati 3500 iwapo kungekuwepo na uwekezaji.

Profesa Muhongo amesema upo uwezekano wa tafiti kuonesha hivyo ila kwa sasa serikali ipo katika harakati za kuleta umeme ambao utaweza kumfikia kila Mtanzania kwa gharama ndogo bila tatizo lolote.

Profesa Muhongo amesema mikakati ya Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 kunakuwepo zaidi ya uniti 2000 za umeme ambazo zinazalishwa hapa nchini hali ambayo itachangia kukuza uchumi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top