Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai adai uchaguzi ni kichekesho kikubwa.
Uchaguzi wa Rais nchini Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho
kikubwa,’ Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema, akituhumu udanganyifu
wa kura uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema uupigaji kura wa Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si halali’.
Kundi kubwa la waangalizi mapema lilisema kufikia hadi watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Chama cha Bw Mugabe ambacho kinadai kushinda, kimekanusha tuhuma hizo kikisema upigaji kura ulikuwa shwari.
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa
zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alisemsa kwenye tathimini yao ya
awali kuwa upigaji kura ulikuwa huru na haki.
Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali ya amani katika uchaguzi huo.
Kuhesabu kura ulianza kulianza usiku na Tume ya
Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ina siku tano za kutangaza nani mshindi
katika uchaguzi huo.
Tayari polisi wameonya kuwa watachukua hatua
dhidi ya yeyote atakayejaribu kuvujisha habari za matokeo. Ni kinyume
cha sheria kutangaza matokeo yasiyo rasmi ambapo vikosi vya ziada baadhi vikiwa na vifaa vya kupambana na waandamanaji tayari viko mjini Harare.
Hatua za kisheria huenda zikafuata sasa, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Andrew Harding akiripoti kutoka Johannesburg.
Lakini megi yatategemea iwapo majirani wa Zimbabwe watapitisha uchaguzi huo, mwandishi wa BBC anaongezi.
'Uchaguzi umekumbwa na kasoro kubwa'
Akizungumza kwenye makao makuu ya chama chake
cha Movement for Democratic Change (MDC) mjini Harare, Bw Tsvangirai
alisema: "Hitimisho letu ni kuwa uchaguzi huu ni kichekesho kikubwa.’
"Uhalali wa uchagauzi huu umeharibiwa na ukiukwaji wa sheria na shughuli za kiutawala ambazo zimeathiri matokeo yake.”
"Ni utani ambao hauonyeshi matakwa ya watu."
Bw Tsvangirai alizungumza muda mfupi baada ya
mtandao wa waangalizi (Zimbabwe Election Support Network-ZESN) kusema
kuwa uchaguzi huo ‘umekumbwa na kasoro kubwa".
Katika taarifa yake rasmi ZESN limesema wapiga
kura muhimu kufikia asilimia 82 walizuiwa katika vituo vya kupigia kura
maeneo ya mijini ambako ni ngome ya Bw Tsvangirai.
Katika maeneo ya vijijini, ambako ni ngome ya Rais Mugabe ni asilimia 38, kundi hilo limeongeza.
Jumatano wanavijiji, mawakala wa MDC kwenye
vituo vya kupigia kura na ZESN walisema kumekuwa na kasoro kadhaa katika
baadhi ya maeneo ya jimbo la Masvingo.
Walisema viongozi wa jadi na wakuu wa vijiji
waliwapanga watu kwenye mistari na kuwalazimisha kutembea kuelekea vituo
vya kupigia kura na kuwapa namba za kupigia kura kama vile kuwahakiki
wamempigia kura nani.
Wanatuhumu kuwa kwenye maeneo haya baadhi ya
watu wasomi walilazimishwa kujifanya hawajui kusoma na kuandika na
wakasaidiwa kupiga kura ambazo zilikuwa ni kwa Zanu-PF.
Msemaji wa Zanu-PF Mtaalam wa Saikolojia Maziwisa alikanusha kuwa wapiga kura wengi wamezuiwa makusudi kujiandikisha. ingawa amekiri kuwapo kwa kasoro kadhaa lakini akafafanua kuwa vyama vyote vimeathirika.
"Ni muhimu kumbuka kuwa hiyo kwa sehemu
ilisababishwa na ukweli kuwa baadhi ya vifaa muhimu Waziri wa Fedha
Tendai Biti, anayetoka chama cha MDC alikuwa," Bw Maziwisa aliiambia
BBC.
"Ukiaangalia hali ya Zimbabwe utakuwa na
hitimisho moja tu. Na hii ni juu ya zaidi ya miaka mine iliyopita
tumefanya jitihada za kutosha kufanya mazingira ya Zimbabwe yawe mazuri
inavyowezekana ili uchaguzi uwe huru na hali.."
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment