Morgan Tsvangirai amekua akisisitiza kwamba uchaguzi mkuu wa Zimbabwe ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.
Morgan Tvangirai anakabiliwa na makosa ya kudharau mahakama kufuatia matamshi aliyoyatoa kuhusiana na idara hiyo.
Jaji wa mahakama kuu Chinembiri Bhunu amesema
waendesha mashtaka watafahamishwa kuhusu tuhuma hizo. Haya yanajiri
wakati chama cha Tsvangirai cha Movement For Democratic Change
kimepoteza kesi mbili kulalamikia uchaguzi mkuu wa Julai 31 mwaka huu.
Mahakama ya kikatiba ilitangaza kwamba Rais
Robert Mugabe alishinda uchaguzi kwa njia huru na haki. Mugabe alipata
asili mia 61 ya kura dhidi ya asili mia 34 alizopata Bw. Tsvangirai.
Viongozi hao wamekuwa katika utawala wa kugawana
madaraka ulioafikiwa mwaka 2009 kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na
utata. Chama cha MDC kiliondoa kesi yake mbele ya mahakama ya kikatiba
kikisema hakikuwa na imani ya kutendewa haki.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment