Katika mkutano huo mbunge huyo aliwataka
wananchi hao kumwombea na kumuunga mkono katika harakati zake za kuwatetea.
"Ubunge wangu na msimamo ni mwiba kwa baadhi ya watu ambao hawapendi
nipate mafanikio... wamekuwa hawalali na wanakesha ili waweze kunimaliza, nasema sintaacha kuwatetea
wananchi wangu eti kwa sababu ya mtu fulani," alisema Aeshi.
Aeshi alisema ubunge wake umekuwa
ukikabiliwa na changamoto nyingi tangu achaguliwe mwaka 2010 ambapo
alifunguliwa kesi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ya kupinga ushindi wake.Alisema anaamini kuwa matokeo ya
kufunguliwa kwa kesi ya kupinga ubunge wake yalitokana na shinikizo la baadhi
ya wakongwe wa siasa ndani ya CCM mkoani Rukwa ambao tangu awali waliapa kuwa
hawezi kupata ubunge, lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu alifanikiwa kuupata.
"Nina uhakika mimi napendwa sana na
wapiga kura wangu, lakini wapo wazee ambao roho yao ni mbaya hawataki kuona
hilo, sasa naomba niwaeleze kupitia mkutano huu kuwa mimi ndiye mbunge halali
wa jimbo hili na nawaomba waniache niweze kushirikiana na wananchi wangu katika
kuleta maendeleo ya jimbo hili," alisema na kuongeza.
"Kwa n i wa n a c h o umi a mimi kuwa
mbunge ni nini?" Alihoji Mbunge huyo. Alisema licha kufunguliwa kesi za
uchaguzi, miezi miwili baada ya kurejeshewa ubunge wake alipewa notisi ya siku
14 na mtu aliyemwita kuwa ni mwanasiasa mkongwe akimtaka kumwomba radhi ndani
ya siku hizo vinginevyo atafikishwa mahakamani na kudaiwa fidia ya sh. milioni
800.
Alisema n o t i s i h i y o inadai kuwa
Mbunge huyo amemdhalilisha mmoja wa wanasiasa wakongwe mkoani Rukwa kwa kumsema
nje na kwenye vikao vya bunge lililopita mara baada ya kurejeshewa ubunge wake
kuwa anamiliki nyumba nane mali ya Serikali ambazo alikodishiwa na Serikali na
yeye akadaiwa kuzikodisha kwa wapangaji wageni kwa bei kubwa zaidi ya ile ya
Serikali.
Aeshi alisema pamoja na notisi hiyo
hataacha kuwatetea wapiga kura wake, kwani anafahamu wapiga kura wake
wamekandamizwa katika maeneo mengi kwa miaka ya nyuma ikiwa ni pamoja na
kudhulumiwa ardhi yao na kuongeza kuwa anawaomba wananchi hao kushikamana ili
malengo yake ya kuwaletea maendeleo yaweze kufanikiwa.
Alisisitiza kwa muda mrefu wananchi wa mkoani Rukwa
wamekuwa wakikandamizwa na hao watu, bahati mbaya hakukuwa na mtu wa kuwaeleza
ukweli wao, lakini yeye ndiye suluhisho la mambo hayo, kwani haogopi na
ataendelea kubomoa kila uovu wao wanaofanya.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment