Picha hizi zilipigwa nchini Norway ambako ilielezwa kuwa gari zina muda wa kuisha muda wa matumizi kama ilivyo kwa dawa za kutibia wanyama. Mmiliki wa gari anatakiwa kuijua tarehe ya gari lake kuisha matumizi ambapo anapaswa kulipeleka gari hilo kwenye kituo maalumu kabla ya tarehe ya mwisho wa matumizi kupita.
Katika gari hilo hakuna kinachochukuliwa zaidi ya kuondoa mipira ya matairi.
Gari hilo, ambalo kimsingi kwa mazingira kama ya Tanzania linaweza kuwa na uwezo wa kutumika, litawekwa kwenye magari mengine chakavu kusubiri siku ya kusagwa ili kupata vyuma kwa ajili ya matumizi mengine.
Maswali ya kujiuliza kwa Tanzania:
Ukija kwa mazingira ya Tanzania kuna mambo mengi ya kulinganisha ambayo yanaweza kuibua maswali mengi.
Je, katika mazingira ya Tanzania ni magari mangapi yapo barabarani lakini yamepita muda wa matumizi? Ni watanzania wangapi wanaweza kumiliki magari mapya? Barabara zetu ni nzuri kwa kiwango cha kutoweza kuzichosha gari mpya mapema? Sheria zinasemaje kuhusu magari chakavu kutumika barabarani? Elimu kwa raia kuhusu kununua gari mpya imetolewa? Watunga sera na wasimamizi wanawajibikaje?
Bila shaka utabaini kuwa utekelezaji wa sheria kama hii kwa mazingira ya Tanzania unakabiliwa na changamoto nyingi. Hata hivyo, bado kuna ya kujifunza ili tutoke tulipo kwa sasa.
Na Azimioblog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment