- Mwenyekiti: FREEMAN MBOWE
- Makamu Mwenyekiti Bara: Profesa ABDALLAH SAFARI
- Makamu Mwenyekiti Zanzibar: SAID ISSA MOHAMED
- Mwenyekiti wa Baraza la Wazee: HASHIM JUMA ISSA
- Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake: HALIMA JAMES MDEE
- Mwenyekiti wa Baraza la Vijana: PASCHAL KATAMBI PATROBAS
Katika uchaguzi huo, Mbowe alipata kura 789 dhidi ya 20 za mpinzani wake.
Prof. Safari ambaye hakuwa na mpinzania, alipata kura 775.
Said alipata kura 645 dhidi ya 163 za Hamad Yusuf aliyekuwa akiwania kiti hicho pia.
Katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili, Septemba 14, 2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mgombea wa kiti cha Uenyekiti Taifa, Kansa Mohamed Mbaruku (Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA mkoa wa Tabora) alijitoa siku moja kabla ya uchaguzi kwa madai kuwa
katiba ya chama hicho imekiukwa hivyo akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.
Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi hiyo.
Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njiaMbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa kwa Mbarouk.
Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.
HASHIM JUMA ISSAMwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA |
HALIMA JAMES MDEEMwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA - BAWACHA |
PASCHAL KATAMBI PATROBAS Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA - BAVICHA |
0 comments:
Post a Comment