Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao walioamua kugawana mke mmoja.
Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya
kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini
mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao ambaye ameieleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja ya wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini walipogunduana, ilikuwa ni ugomvi wa
mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao,
alishindwa ndipo akasema anawapenda wote wawili.
Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini
mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama
bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda
kumjulia hali.'
Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana
majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na
kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni
haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa
umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa
kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment