Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), jana iliridhia
kumvua uanachama, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini
Magharibi, Mansour Yussuf Himid kutokana na kukiuka miiko ya chama
hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye
aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa Mansour ambaye
hivi karibuni alikuwa waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ), amefukuzwa uanachama kutokana na kukiuka mambo matatu.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni kushindwa kutimiza
malengo ya CCM na kutekeleza malengo ya uanachama, kushindwa kutekeleza
wajibu wa uanachama na kukiuka maadili ya uongozi, kuikana na kuisaliti
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.
Kutokana na uamuzi huo, Nape alisema Mansour
hatakuwa na nafasi ya kukata rufani mahali popote kwa kuwa uamuzi
uliofikiwa jana ni wa kikao cha juu na cha mwisho.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mansour alisema kwa
sasa hawezi kuzungumza mengi kwani anahitaji muda wa kutafakari
kutokana na uzito wa suala lenyewe.
“Ndugu yangu nashukuru sana kwa kunipigia simu.
Ila ninahitaji muda wa kutulia kwanza. Nipe kama siku mbili au tatu hivi
halafu nitaongea,” alisema Mansour, ambaye amekuwa Mwakilishi wa Kiembe
Samaki tangu mwaka 2005.
Nec ilifikia uamuzi huo ikibariki mapendekezo
yaliyotolewa na Kamati Kuu ya CCM upande wa Zanzibar iliyomvua uanachama
kutokana na misimamo yake ya kisiasa na hasa suala la Muungano.
Mansour aliwahi kushika nyadhifa kadhaa ndani ya
CCM ikiwamo ya ujumbe wa Halmashauri Kuu na Mweka Hazina wa chama hicho
upande wa Zanzibar.
Kilichomponza
Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansour zilifikishwa
katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Zanzibar, kilichoketi Agosti
16, mwaka huu katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambacho wajumbe wa kamati
hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfuta uanachama.
Suala hilo lilifikishwa Kamati Kuu ya CCM,
Zanzibar Agosti 22, mwaka huu kupitia uamuzi huo na iliafiki. Kitendo
cha Mansour kuingia kwenye Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar inayoongozwa
na mwanasiasa mkongwe Hassan Nassor Moyo ambayo imekuwa ikipigania
Muungano wa mkataba ilichochea tofauti yake na makada wenzake wa CCM
Zanzibar.
Kitendo cha kuungana na Mzee Moyo na Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad kupigia debe suala la
Muungano wa Mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar kuliwakera makada wa
CCM waliomchukulia kuwa anapingana na Katiba na Ilani ya CCM
vilivyosimamia katika Serikali mbili.
Nyadhifa SMZ
Bukoba ngoma nzito
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Nyadhifa SMZ
Mansour, ambaye amekuwa Naibu Waziri wa Maji,
Nishati, Ardhi na Mazingira kuanzia mwaka 2000-2005. Alipanda cheo na
kuwa waziri kamili katika wizara hiyo kuanzia mwaka 2005 hadi 2010
alipohamishwa kuwa Waziri wa Kilimo kati ya 2010 na 2012 na Aprili,
mwaka jana aliteuliwa kuwa waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu na Mjumbe
wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
Hata hivyo, hakudumu muda mrefu katika wadhifa huo
kwani alivuliwa wadhifa huo kutokana na kile kilichokuwa kimeelezwa
tangu awali kwamba ni kutofautiana na chama hicho.
Nyota yake iling’ara zaidi alipokuwa Wizara ya Nishati akiwa naibu na baadaye waziri kamili kwani alikuwa mmoja wa wanasiasa wa Zanzibar waliopinga waziwazi suala la mafuta kuingia kwenye masuala ya Muungano na hasa kwenye mijadala ya Baraza la Wawakilishi.
Nyota yake iling’ara zaidi alipokuwa Wizara ya Nishati akiwa naibu na baadaye waziri kamili kwani alikuwa mmoja wa wanasiasa wa Zanzibar waliopinga waziwazi suala la mafuta kuingia kwenye masuala ya Muungano na hasa kwenye mijadala ya Baraza la Wawakilishi.
Bukoba ngoma nzito
Kwa upande wa sakata la mgogoro wa Bukoba, Nape
alisema Kamati Kuu itaendelea kuwahoji wahusika hao leo baada ya
kushindwa kukamilisha kazi hiyo jana.
Suala hilo linawapambanisha vigogo wa siasa wa
Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mbunge wa Bukoba Mjini, Khamis Kagasheki
na Meya, Dk Anatory Amani.
“Suala la Bukoba tutaendelea nalo kesho (leo) saa
tano asubuhi baada ya kutokukamilisha kazi yake leo (jana), hivyo Kamati
Kuu inatarajia kuendelea kushughulikia mgogoro huo kabla ya kuondoka
mjini Dodoma,” alisema Nape.
Mbali na kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya Katiba,
Halmashauri Kuu pia ilipitisha majina ya makatibu watatu wa CCM ngazi ya
mikoa.
Waliopitishwa ni Mary Maziku, Romuli Njovu na
Kassimu Mabrouk ambao watapangiwa mikoa. Pia ilipitisha uteuzi wa
makatibu 25 wa wilaya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Mwananchi
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment