Serikali ya
Tanzania na China zimeandaa mdahalo ambao utahusisha nchi mbalimbali ukiwa na
lengo la kujadili fursa za ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ambapo fursa
ya ndoto ya china katika kuleta
maendeleo Tanzania na kuimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania katika hali
ambayo kila upande utanufaika.
Mshauri wa masuala
ya kisiasa wa Balozi ya China Nchini Tanzania Bwana Li Su Hang amesema ni fursa
nzuri kwao kueleza mawazo yao katika ndoto yao katika Afrika kimaendeleo.
Na kaimu naibu mkuu wa chuo kikuu cha Dar Es
Salaam Profesa Bonivecha Rutinwa ameeleza malengo manne ya mdahalo huo ambayo ni fursa ya ndoto ya China katika kutimiza malengo yao
kwa Tanzania, muelekeo wa pamoja kati ya Afrika na China katika kutimiza malengo
yao, fursa na changamoto katika ushirikano kati ya China na Tanzania katika
mustakabali mpya na jinsi ya kuimarisha uhusiano katia ya China na Tanzania
katika hali ambayo kila upande utanufaika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment