Wafuasi wa Morsi wakiandamana nje ya msikiti wa  Rabaa al-Adawiya Square, Julai 27, 2013. 
Wafuasi wa Morsi wakiandamana nje ya msikiti wa Rabaa al-Adawiya Square, Julai 27, 2013.
 
Wafuasi wa rais aliyeng’olewa madarakani  nchini Misri Mohammed Morsi wameapa kuendelea na maandamano, licha ya onyo kutoka kwa waziri wa maswala ya ndani  kuwa serikali inajiandaa kuvunja maandamano hayo mjini Cairo ambayo yameendelea kwa wiki kadha sasa.
Malefu ya wafuasi wa Morsi walisimama kidete katika maeneo mawili ya maandamano, moja nje ya miskiti wa Raba’a al-Adawiya na nje ya chuo kikuu cha Cairo,siku moja baada ya waandamanaji kuzozana na vikosi vya  ulinzi ambapo  zaidi ya watu 74 waliuawa na takriban 800 kujeruhiwa.

Waziri wa maswala ya ndani Mohamed Ibrahim alisema anatumaini maandamano hayo yatavunjwa bila kusababisha maafa mengi na kwamba “kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, sharti yakome.”

Baadhi ya watu wanaounga mkono waandamanaji walisema wanaanza kuona hatari inayowakabili.Kundi la Muslim Brotherhood la Morsi linasema polisi na watu wengine waliojihami walifytaua risasi na kuuwa waandamanaji.

Lakini maafisa wa Misri wanakanusha madai hayo wakisema polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na kwamba wafuasi wa Morsi wanawajibika kwa ghasia hizo. 
Chanzo: VOASwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top