Chama Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimewapongeza wananchi wa Arusha kwa kujitokeza kupiga kura ambazo zimekiwezesha chama hicho kuibuka na ushindi wa kata zote nne.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dakta Slaa ametoa wito kwa wananchi kujikita katika shughuli za uzalishaji mali badala ya kuyumbishwa na wanasiasa ambao mara nyingi huvutia kwenye maslahi yao kisiasa.

Katibu mkuu huyo amesema anaamini chama chake kipo imara kukabiliana na upinzani mkali kutoka chama tawala na vyama vingine hivyo wanaamini uchaguzi mkuu mwaka 2015 watafanya vizuri zaidi.

Kwa upande wa katibu wa uenezi wa chama cha mapinduzi CCM Nape Nnauye amesema kuwa kushindwa kwa chama chake sio suala la kuwalaumu CCM Makao makuu.

Naye Mhadhiri mwandamizi wa masuala ya sayansi ya Siasa wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Dakta Mohamed Bakari ametoa rai kwa CHADEMA kuwa na mazingira mazuri ya kisiasa.

Dakta Bakari ametoa angalizo kwa CCM kuwa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, chama tawala lazima kikubali mabadiliko vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya zaidi mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.
 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top