Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
1/06/2013.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
imepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii
wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko
Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za
muziki, Jumanne tarehe 28 Mei, 2013.
Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa
kwa fani ya muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri
wake katika fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya
uimbaji ya "Free Style" alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani
na nje ya nchi.
Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.
Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.
Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
"Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangwea mahala pema peponi."
Imetolewa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara.
0 comments:
Post a Comment