UPATIKANAJI WA HATI ZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YALIYOTANGAZWA UPYA

Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Nne Oktoba, 2012 kwamba Hati za Matokeo (Notification of Examination Results) zilizotolewa baada ya matokeo kutangazwa upya zitapelekwa shuleni/kwenye vituo walikofanyia mtihani

Hivyo, watahiniwa wanaombwa kuwasiliana na Wakuu wa Shule/Vituo vyao vya mtihani ili waweze kukabidhiwa hati zao kuanzia tarehe 20 Juni 2013

Hati za matokeo zilizotolewa mwanzoni (mwezi Machi, 2013) zimebatilishwa kwa sababu matokeo ya awali yaliyomo kwenye hati hizo yalifutwa.

Tanbihi
Kila mtahiniwa atapaswa kuwasilisha hati ya matokeo ya awali kwa Mkuu wa Shule/Kituo kabla ya kupewa hati mpya.
Limetolewa na:
 Katibu Mtendaji
Baraza la Mitihani la Tanzania

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top