Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya
Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya
kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huoleo Juni 6, 2013. Wa pili kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison
Mwakyembe (wa tatu) kulia.
Mojawapo ya
vivutio vikubwa katika jiji la Singapore ni hoteli hii ya kitalii na
casino iitwayo Marina Bay ambayo kuna jengo la mgahawa lenye umbo la
meli juu ya majengo yake mawili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake
wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji
Upya ya Singapore leo Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo
ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na
kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika
picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya
Singapore leo Juni 6, 2013.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu ya ufundi
(Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa Tanzania leo
Juni 6, 2013 ambapo pamoja na mambo mengine walijionea jinsi wanafunzi
wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja
na vya ndege.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe
wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya
Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa
umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa
kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake
katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa
miji ya Singapore leo Juni 6, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi
wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea kampasi
yao jijini Singapore leo Juni 6, 2013.
PICHA NA IKULU
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment