RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein
ameeleza kuwa azma ya Indonesia ya kuzidisha mashirikiano na Zanzibar
katika uimarishaji wa sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kwa
kutoa nafasi za masomo nchini humo kutasaidia kufikia lengo lililowekwa
katika sekta hiyo nchini.
Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mbe. Zakaria Anshar, Ikulu mjini Zanzibar.
Katika
maelezo yake Dk. Shein alimueleza Balozi Anshar kuwa hatua hiyo
itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha sekta ya elimu nchini
pamoja na kuwapatia nafasi za masomo vijana wa Kizanzibari.
Dk.
Shein alisema kuwa juhudi za makususdi zimekuwa zikichukuliwa na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu hasa
elimu ya juu, hivyo azma ya Indonesia kusaida kuiunga mkono Zanzibar kwa
kutoa nafasi za elimu ya juu kutasaidia kwa kiasi kikubwa uimarishaji
sekta hiyo.
Pamoja
na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa uhusiano huo katika sekta ya elimu
utaimarika zaidi kwani wanafunzi kutoka nchini humo nao pia watapata
nafasi ya kuja kujifunza Kiswahili hapa Zanzibar pamoja na kuimarisha
uhusiano na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Akizungumza juu ya sekta nyengine ambazo Indonesia imeahidi kutoa mashirikiano yake kwa kuiunga mkono Zanzibar ikiwemo sekta ya afya, utalii, utamaduni, biashara na kilimo Dk. Shein alisema kuwa hatua hiyo ni jambo la busara.
Kwa
upande wa sekta ya kilimo, Dk. Shein alisema kuwa kutokana na nchi hiyo
kupata mafanikio katika sekta hiyo hasa katika kilimo cha mpunga,
kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mashirikiano katika sekta ya
kilimo hapa nchini.
Kwa
upande wa sekta ya biashara, Dk. Shein alisema kuwa Indonesia ina
historia kubwa ya kibiashara kati yake na Zanzibar, hivyo hatua hiyo
itaimarisha zaidi sekta hiyo hasa biashara ya karafuu. Pia, Dk. Shein
alieleza kuwa kutokana na nchi hiyo kuwa na vivutio mbali mbali vya
utalii pamoja na uzoefu mkubwa walionao sambamba na tamaduni za nchi
mbili hizi kulingana kutaweza kutoa mashirikiano kwa pande mbili hizo
kwenye sekta hiyo.
Aidha,
katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo mikakati
iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta
zake za maendeleo na kuipongeza Indonesia kwa azma yake ya kuiunga mkono
Zanzibar.
Nae Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Bwana Zakaria
Anshar, alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake ina inathamni uhusiano na
ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati yake na Zanzibar na kusisitiza kuwa kuwepo kwa Ubalozi wa nchi hiyo hapa Tanzania kutarahisisha zaidi mashirikiano pamoja na uhusiano huo.
Mhe. Anshar alisema kuwa Indonesia
imeamua kwa makusudi kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za
maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kwa kutoa nafasi za kujiunga katika
vyuo vya elimu ya juu nchini Indonesia pamoja na kushirikiana na vyuo
vya hapa nchini.
Akieleza
mafanikio yaliopatikana kwenye sekta ya kilimo, Balozi huyo alisema
kuwa Indonesia imeweza kupata mafanikio makubwa katika sekta hiyo hasa
katika kilimo cha mpunga ambapo itakuwa ni fursa ya pekee kutoka
utaalamu wake kwa Zanzibar.
Kwa
upande wa sekta ya biashara, Balozi huyo alieleza kuwa mbali ya
biashara ya karafuu, pia, ushirikiano huo utawasaidia wafanyabiashara
binafsi kutoka Zanzibar kwenda nchini humo kwa ajili ya kununua bidhaa
tofauti na wale wa Indonesia kuja Zanzibar.
Wakati huo huo, Dk. Shein alifanya mazungumzo na Balozi wa Denmark anayeshughulikia mashirikiano na maendeleo duniani Mhe. Bibi Charlotte Slente aliyefuatana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Johnny Flento huko Ikulu mjini Zanzibar na kuzungumza masuala mbali mbali yanayohusu sekta ya afya.
Katika
mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar
imejiwekea mikakati maalumu katika kuhakikisha sekta ya afya inaendelea
kupata mafanikio makubwa.
Dk.
Shein alimueleza Balozi huyo kuwa licha ya kuungwa mkono na Washirika
mbali mbali wa Maendeleo ikiwemo Denmark, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
imeweka kipaumbele zaidi katika uimarishaji wa sekta ya afya.
Nae Bi Charlotte
Slente alimuhakikishia Dk. Shein kuwa Denmark itaendelea kuiunga mkono
Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya hasa ikizingatia juhudi
inazozichukua katika kuimarisha sekta hiyo.
0 comments:
Post a Comment