Police1 5efd4Jeshi la Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27 Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83, yenye kichwa cha habari "MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW".

Taarifa hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na ugonjwa wake wa akili.

Jeshi la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye lengo la kupotosha jamii.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top